Hii
ni idara kati ya idara tisa (9) zilizopo katika casfeta mkoa wa Tanga. Idara
hii hapo mwanzo haikuwepo, kuanzishwa kwa idara hii ya ict (Teknolojia, Habari
na Mawasiliano) ilianza mwaka March, 2017 katika tawi la Casfeta Chuo Cha
Ualimu Korogwe (TTC) tawi lililopo wilaya ya Korogwe mjini. Wazo la kuanzishwa
kwa idara hii liliibuliwa na Mwenyekiti
wa tawi la Casfeta (TTC) Korogwe mjiini siku chache kabla ya kufanyika
tamasha kubwa la kusifu na kuabudu lililofanyikia tawini hapo likihudhuliwa na
watu toka makanisa mbalimbali na vikundi vingine vya kidini vilivyopo chuoni
hapo. Idara hii ilianziahwa kwa lengo la kutunza taarifa kwa njia ya
kielectronic zikiwemo taarifa za tawi, kuchapa barua kwa kutumia computer,
kutengeneza matangazo mbalimbali, kurekodi na kuhifadhi matukio mbalimbali
zikiwemo ibada na makusanyiko mengine.
Baada
ya siku chache kiongozi huyo alichaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Casfeta
wilaya ya Korogwe pia akapendekeza kuwepo na idara hii ya ict kulingana na
umhimu wake na faida ambayo iliyokuwa imeonekana kwa muda mfupi hapo tawini.
Hivyo kwa madhumuni yale yale, liliongezwa wazo jingine la kufungua website pamoja
na blog ya Casfeta wilaya ya korogwe. Mwenyekiti aliwachagua viongozi wa idara
hii wenye utaalamu na masuala ya mitandao na computer programming wakiwemo
mwenyekiti Lazaro Chingula, mwenyekiti msaidizi Erick John na Meshack Muna kama
katibu wa idara.
Pia
kwenye tamasha la pasaka mkoa wa Tanga lililofanyika mwezi wa nne mwaka 2017
wilayani korogwe, walichaguliwa viongozi wa casfeta mkoa wa Tanga ambapo Samwel
Erasto alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa casfeta
mkoa wa Tanga 2017/2018.
Mara
baada ya kukabidhiwa majukumu alitangaza moja kwa moja kuanzishwa kwa idara ya
ict mkoa wa Tanga. Aliwachagua na kutangaza viongozi wa idara hii ambapo
aliwachagua na kuwatangaza viongozi wafuatao:-
Mwenyekiti
– Lazaro Chingula
M/msaidizi
– Erick John
Katibu
– Meshack Muna
MAJUKUMU NA MALENGO MAKUU YA IDARA
YA ICT
i)
Kuwaunganisha wana – casfeta mkoa wa
Tanga, walezi, wachungaji na wadau mbalimbali wa casfeta nje na ndani ya
casfeta mkoa wa Tanga kwa njia ya mitandao.
ii)
Kusambaza habari kwa njia ya mitandao.
Zikiwemo matangazo ya mkoa, habari ya kielimu, taarifa za mitihani, matokeo
kuanzia kidato cha kwanza hadi chuo.
iii)
Kurekodi na kutunza kumbukumbu kwa njia
ya kielectonic.
iv)
Kutoa elimu kwa wana – casfeta na wadau
mbalimbali juu ya faida na athari za mitandao na ukuaji wa teknolojia kwa
kanisa la leo, hasa kwa vijana wa kizazi cha doti komu (kizazicha.com).
v)
Kukuza na kuongeza kipato ndani ya
casfeta mkoa wa Tanga na kuondoa au kupunguza hali ya utegemezi. (idara hii
itatumika kama mradi wa kuingiza kipato ndani ya mfuko wa casfeta mkoa wa
tanga).
vi)
Kuwaimarisha wana – casfeta kiimani na
hali ya kumtegemea Mungu kwa kuutunza wokovu pasipo mawaa kwa kupitia vipindi mbalimvbali
vitakavyo endeshwa mtandaoni na
kuwafikia wana – casfeta popote walipo.
MBINU ZITAKAZO TUWEZESHA KUTIMIZA
MALENGO
Nje
na malengo ya kuanzisha casfeta Blog idara iliona mbali ikaamua pia kuanzisha
CASFETA TV (Casfeta Online TV) ambayo itakuwa inarusha matangazo ya moja kwa moja
yakiwemo makusanyiko ya Jointmass, December conference, mafundisho mbalimbali
ya vijana yatakayo kuwa yanafundishwa na wachungaji mbalimbali pamoja na walezi
wa casfeta mkoa na wilaya zake pia pamoja na makusanyiko mengine muhimu
yakiwemo makusanyiko yanayofanyika makanisani pamoja na makusanyiko yanayohusu
elimu kwani casfeta ni chombo kinachowaongoza wanafunzi waliopo mashuleni na
vyuoni hivyo kuna ulazima na umuhimu wa kipekee wa kujua masuala ya kielimu.
Yakiwemo:-
·
Uchaguzi wa combination kulingana na
taasusi ya kutaka kusomea hapo baadaye
·
Sifa za kujiunga na vyuo mbalimbali
·
Kupata matokeo mara baada ya kutangazwa
na wizara husika yakiwemo matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha
sita pamoja na uchaguzi wa kujiunga na vyuo mbalimbali.
MAHITAJI YALIYOMO NDANI YA IDARA
Kama
Casfeta Blog na Casfeta TV ni chombo kinachosimamiwa na idara ya ICT
(Teknolojia, Habari na Mawasiliano) chini ya uongozi wa casfeta mkoa wa Tanga.
Hivyo kama mdau unaweza kudonate kwenye blog yetu ili kusaidia huduma hii
pamoja na ununuzi wa vifaa vifuatavyo.
·
Computer
·
Camera
·
Smartphone
·
Tablet
·
Empty DVD/CD
·
Pamoja na vifaa vingine vingi vya
kielectronic vitakavyo tusaidia kuendesha Casfeta Blog na Casfeta TV mkoa wa
Tanga.
UMILIKI WA CASFETA BLOG &
CASFETA TV
Casfeta
Blog & Casfeta TV Mkoa wa Tanga daima inamilikiwa na Casfeta Mkoa wa Tanga,
ambapo Mwenyekiti ndiye kiongozi mkuu wa Casfeta Blog & Casfeta TV chini ya
Mkurugenzi wa Casfeta Mkoa wa Tanga, wachungaji pamoja na walezi.
Kama
ilivyo idara zingine mwenyekiti atahusika uteua na kuwatangaza viongozi ambao
watakuwa wakiendesha Casfeta Blog & Casfeta TV kipindi chote cha uongozi
wao.
Pia
Mwenyekiti wa idara atawajibika kuchagua waendeshaji/watayalishaji wa vipindi
mbalimbali vinavyorushwa na Casfeta Blog & Casfeta TV kutoka kila wilaya
zilizomo mkoa wa Tanga.
0 comments:
Post a Comment